DRC

Rais wa Congo DRC Felix Tshisekedi afanya mabadiliko ya juu katika jeshi lake

DESEMBA 20, 2024
Border
news image

Katika tangazo lililo somwa kupitia televisheni ya taifa, Rais wa DRC Felix Tshisekedi ameteua kiongozi mpya wa jeshi Luteni Generali Jules Banza Mwilanie kuwa mkuu wa jeshi la taifa, akimgomboa mwenize Christian Tshiwewe Songesha ambaye ameteuliwa kuwa mshauri wa kijeshi wa Rais wa nchi.

Pamoja na hayo, mabadiliko mengine yamefanyika katika uongozi wa mkuu wa jeshi la ardhini na ujasusi, sababu kubwa ya kubadilisha viongozi hao ikiwa bado haijulikane ila, wakaazi wakilalamikia mara kwa mara viongozi wa jeshi la Congo katika operesheni za kijeshi mashariki mwa taifa hili kubwa Afrika ya Kati na Maziwa Makuu.

Wakaazi wanaopatikana katika vijiji vinavyoikaliwa na waasi wa M23 kwa muda mrefu wakiomba viongozi hao kuwajibika na kuhakikisha usalama unarudi kwenye mikoa, miji na vijiji mbali mbali ambavyo zaidi ya miaka miwili sasa vinadhibitiwa na M23 ambayo serikali yasema inaungwa mkono na serikali ya Rwanda.

Mapigano kati ya M23 na jeshi la serikali imesababisha watu zaidi ya milioni saba kuwa wakimbizi wa ndani katika taifa lao, wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kusababisha vijana wengi kujiunga na makundi ya wapiganaji kama wazalendo na wengine M23.

DR Congo kwa sasa inashuhudia vikosi vingi hasa kutoka MONUSCO, SADC na wanajeshi wengine kutoka Burundi na Ulaya ambao waunga mkono serikali ya Kinshasa lakini bado uasi ukiendelea kushikilia vijiji na kuzuia wakaazi kuendelea na kazi zao za kawaida pamoja na kuwa wakimbizi katika kambi ama katika familia mbali mbali pembezoni mwa Mji wa Goma, katika Miji ya Butembo na Beni.

AM/MTV News DRC