DRC

Rais Wa Congo Afanya Uzinduzi Wa Miradi Mbali Mbali Katanga

OKTOBA 03, 2023
Border
news image

Rais felix Tshisekedi wa DRC afanya Uzinduzi wa miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa barabara Kasomeno-Kasenga-Chalwe, hii imefanyika katika ushinikizwaji wa Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde akitoa heshima kwa Rais FĂ©lix Tshisekedi na mwenzake wa Zambia Hakainde Hichilema ambao wamekubaliana kuunganisha mataifa yao mawili kupitia daraja kubwa kati ya Congo DRC na Zambia.

Barabara itakayo unganisha mataifa ya Africa Kusini na DRC hasa eneo lake la Katanga ikiwa eneo muhimu kwa biashara.pande zote zimesema kazi hizi zinaweza fanya miaka mitatu iwapo nguvu zote zitatumika vilivyo.

Hii imejiri wakati ambapo Rais wa Congo yuko katika wilaya na mikoa mbali mbali ya Katanga ya zamani ikiwa mikoa inayo kuwa na mali mengi lakini raia wake wakishuhudia Maisha magumu.

Rais wa Congo amesema lengo lake kubwa nikuona raia wa Congo anafaidika kwa raslimali ya taifa lake.

AM/MTVNEWS