DRC

Rais wa Burundi Ndayishimiye awasili Mjini Kinshasa Congo DRC kwa ziara ya siku mbili

AGOSTI 27, 2023
Border
news image

Kwenye ukurasa wake wa Twitter ikulu ya Rais wa Congo imesema Rais wa Burundi amewasili Mjini Kinshasa kwa ziara ya siku mbili huku akikutana na mwenzie wa Congo DRC Felix Tshisekedi, mataifa hayo mawili inatarajia kuweka makubalinao ya kijeshi kati ya mataifa hayo mawili, makubaliano ambayo itaweka uhusiano bora kati ya vyombo vya usalama vya DRC na taifa ma Burundi.

Burundi ipo DRC katika jeshi la Africa mashariki, na taifa hilo limekuwa likishinikiza mchakato wa amani na usalama mashariki mwa Congo.

Kikosi cha Burundi kipo wilayani masisi Kivu kaskazini ambako bado waasi wa M23 wandelea kutekea vijiji chini ya uangalizi wa wanajeshi wa Africa mashariki ikiwemo Burundi, Kenya, Sudan Kusini, na Uganda.lakini wanajeshi hao wakilalamikiwa na wananchi kuwa wanashirikiana na M23 na kushindwa kuhudumisha usalama wa wakaazi, japo wanajeshi hao walitemewa zaidi.

Wanajeshi wa Africa mashariki wana wanajeshi wao wilayani Masisi, Rutshuru na Nyiragongo eneo zinazo dhibitiwa na M23 kama njia moja ya kuepusha pande zinazo kupigana kusitisha mapigano kati yao.

M23 ikoomba mazungumuzo ya moja kwa moja na serikali lakini serikali ya Kinshasa ikiomba M23 kusalimisha silaha zao na kuingia katika mchakato wa P-DDRRCS.

AM/MTVNEWS