MAREKANI

Rais Mstaafu wa Liberia Sirleaf Ampongeza Rais Dk. Samia kwa Kulinda Usawa

SEPTEMBA 23, 2023
Border
news image

Mbunge wa Viti Maalum kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Neema Lugangira ambaye pia ni mwakilishi wa Tanzania katika Mtandao wa Dunia wa Viongozi Wanawake Wanasiasa (Women Political Leaders Org), ameshiriki mjadala wa Usawa wa Kijinsia katika Siasa, mkutano uliofanyikia New York Marekani.

Kufuatia mchango wake na jitihaza za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan alialikwa na Mhe Rais Mstaafu wa Liberia, Ma Ellen Sirleaf katika kikao cha faragha ambapo Mhe Rais Mstaafu Sirleaf amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuiongoza Tanzania kwa kuzingatia Demokrasi na kuimarisha usawa wa kijinsia katika siasa na huduma za kijamii.

Oliver G Nyeriga - MTV