DRC - Beni Kivu Kaskazini

Raia wasio pungua 4 wame fariki Dunia baada ya kuwawa na wapiganaji wa ADF na muasi mmoja kutekwa na wanajeshi wa Fardc-Updf wakati wa shambulizi jipya Karibu na Mji wa Kikingi eneo la Rwenzori

SEPTEMBA 25, 2023
Border
news image

Raia wengi kutoka Kijijini kabisa karibu na Mji wa Kikingi katika sekta ya Ruwenzori , wame toroka Mji wao na kuelekea tarafani watalinga ni wilayani Beni baada ya makaazi yao kushambuliwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni ADF ambao wame waua watu nne na wengine kutekwa hadi misituni.

Mkuu kiongozi wa tarafa la watalinga Pascal BALITUSUKA , ame dhibitisha vifo vya watu 3 ku uawa 3 na wengine kutekwa na kubebwa musituni na muasi mmoja wa kundi la ADF kutekwa na wanajeshi wa Kongo Fardc ,Jeshi la Uganda Updf limefanikiwa kuwanyanganya silaha 1 waasi hao, Kiongozi huyo anasems .Juhudi zina fanywa kufatilia waasi.

Wakati huo , kiongozi wa kirai katika sekta ya Ruwenzori Bwana Meleki Mulala , alesema matokeo ya muda hadi sasa ni Raia 4 ambao wame uawa miongoni mwao wanawake 4 kuna Pia mtu mmoja aliye Jeruhilwa.

Hili likiwa ni shambulizi la Pili katika maeneo ya Kikingi katika kipindi cha Siku Tano.

Wakati UPDF na jeshi la Congo FARDC wanajaribu kuhakikisha wanaokoa watu wanao tekwa na ADF wilayni Beni.

Eriksson LUHEMBWE/MTV BENI