NAIROBI, KENYA

Raia wa Poland Akamatwa Akiwa na Heroini ya Shilingi Milioni 3.2 Katika Uwanja wa Ndege JKIA

SEPTEMBA 15, 2023
Border
news image

Maafisa wa upelelezi wa kupambana na mihadarati katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wamefanikiwa kunasa dawa za kulevya aina ya heroini zenye thamani ya Shilingi milioni 3.2 za kenya na kumkamata mlanguzi huyo, raia wa Poland.

Mshukiwa aliyetambuliwa kama Arkadiusz Stanislaw, mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa katika Kituo cha 1C cha JKIA muda mfupi kabla ya kupanda ndege ya Misri inayoelekea Hungary.

Kulingana na polisi, dawa hizo zilipatikana zikiwa zimefichwa kwenye mizigo yake.

Mlanguzi huyo amesafirishwa hadi katika mji mkuu wa Hungary (Budapest) atashtakiwa kwa kumiliki na kusafirisha mihadarati.

Mnamo mwaka wa 2019, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya Simon Mordue alisema bandari ya Kenya ya Mombasa ilichangia asilimia 30 ya heroini haramu iliyoingizwa katika soko la EU.

Alisema pia kiasi kikubwa cha heroini kinachoingia nchini ,hutoka Afghanistan kupitia Bahari ya Hindi huku cocaine ikitokea Amerika Kusini.

Kukamatwa kwa Stanislaw kumejiri wakati ambapo msako mkali dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya na watengenezaji pombe bila leseni umeongezeka, hatua ya serikali kuzuia biashara hiyo haramu nchini.

Baadhi ya Wakenya wametiwa mbaroni wakiwa na mihadarati nchini India na hivyo kuzua wasiwasi kwamba kunaweza kuwa na dawa hizo nyingi zaidi nchini humo.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kupambana na Dawa za Kulevya Margaret Karanja anaonya kwamba wale wote wanaonaswa na wasafirishaji haramu na wachuuzi watashughulikiwa kwa ukali wa sheria, licha ya majukumu yao katika biashara hiyo.

Dennis Chisaka - Nairobi, Kenya