DRC WAMBUTI / MBILIKIM

Raia kutoka Kabila la mbilikimu ama wambuti nchini DRC waomba serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ku tekeleza sheria zilizo wekwa kwa ajili yao na ku rejesha usalama kwenye eneo lao la asili kwani kwa sasa wapitia hali Ngumu kambini na Mjini

AGOSTI 24, 2023
Border
news image

Raia kutoka Kabila la mbilikimu ama wambuti nchini DRC waomba serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ku tekeleza sheria zilizo wekwa kwa ajili yao na ku rejesha usalama kwenye eneo lao la asili kwani kwa sasa wapitia hali Ngumu kambini na Mjini.

Wambuti ama wabatwa wamesema hayo wakati wakisherekea siku kuu ya kimataifa iliyo wekwa kwa ajili yakabila za asili,mbilikimu wa mkoa wa kivu kaskazini wana laumu hali wanayo pitia kwa sasa mashariki mwa Congo ambako wana kumbana na changamoto za ukosefu wa usalama na kulazimika kuhama makaazi yao ya asili na kuwa wakimbizi pasipo kutaka kwao. Tulio kutana nao wana eleza ya kwamba wame porwa ma shamba Pamoja na wanawake kubakawa na ku kosa mahali pa ku kaa wa ki baki katika hali ya ukimbizi huku waki pitiya hali mbaya kama ukosefu wa vyakula,mavazi na matibabu.

Mbilikimu hao wameomba serikali kurejesha usalama katika eneo zote wanamo ishi ili wa rudi katika misitu na ku ishi Maisha ya kawaida na ku linda mazingira. Lakini hata hivyo wameomba kushirikishwa katika uongozi wa taifana hata kuajiriwa na serikali.

Baadhi yao Waki shukuru Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ku weka sheria inayo tetea haki zao, ila wakiomba utekelezwaji wa sheria hizo ili waishi kama mkongomani yeyote. Pamoja na hayo wameomba kukubaliwa ama serikali kujenga shule kwa ajili yao .

Uta fahamu kwamba siku kuu kimataifa kwa ajili ya makabila ya asili ina sherekewa tariki 9 ogasti ya kila mwaka,mwaka huu wa 2023 Katika mkoa wa kivu kaskazini ili sherekewa hii juma tanu tariki 23 ogasti Mjini Goma na mbilikimu kutoka maeneo mbali mbali.

MTV/News