DRC - BENI

Raia 2 wauawa katika shambulizi jipya la ADF Eneo la Eringeti Kivu kaskazini mashariki mwa Congo DRC

AGOSTI 20, 2023
Border
news image

Shambulizi hilo la kushitukiza lili tekelezwa majira ya asubuhi juma mosi Ogasti 19 katika Kata la Baungachu Luna mjini Eringeti , ni kilomita 60 kaskazini mwa jiji la Beni .

Bwana lewis Saliboko mtetezi wa haki za binadamu toka shirika la "asadho" , amesema kuna raia 2 walio uawa wa jinsia ya kiume na mwanamke mmoja ku jeruhiwa vibaya .

Familia kadhaa kwa kuhofia usalama wao ziliondoka na kuelekea mjini oicha , unao patikana kilomita 30 kusini mwa mji wa Eringeti wilayani Beni .

Muwakilishi wa liwali mkowani Kivu kaskazini sehemu hiyo , bwana NGUOMOJA SABITI ame dhibitisha tukio hilo , na kuongeza yakuwa wapesi wa Jeshi la Kongo uli zuia madhara zaidi . Na kufanyikiwa kukomboa raia 7 waliokuwa tayari wame bebwa na waasi hao , hali imejaribu kuwa tulivu ila raia wengi wame ondoka mjini . alisema kiongozi wa mji wa Eringeti .

Eriksson Luhembwe MTV/Beni