TANZANIA

Naibu Waziri Mkuu Na Waziri Wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko Ameongoza Kikao Cha Kujadili Mikakati Ya Upatikanaji Wa Mafuta Ya Petroli Nchini

SEPTEMBA 11, 2023
Border
news image

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ameongoza kikao cha Kujadili Mikakati ya upatikanaji wa Mafuta ya Petroli nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha tarehe 11 Septemba, 2023 Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja (PBPA)

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania