TANZANIA

Naibu Waziri Mkuu Na Waziri Wa Nishati Atembelea Mradi Wa JNHPP

SEPTEMBA 16, 2023
Border
news image

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko leo Septemba 16, 2023, ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project nchini Tanzania ( JNHPP) ambao ujenzi wake umefikia asilimia 91. 72, huku bwana likiwa na ujazo wa mita 164.81 sawa na lita bilioni 14.66 sawa na asilimia 47.8.

Katika ziara hiyo ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Maharage Chande na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania