TANZANIA

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko Kufungua Maonesho ya Sita ya Madini Geita Tanzania

SEPTEMBA 21, 2023
Border
news image

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati nchini Tanzania Dkt.Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Sita ya teknolojia ya Madini mkoani Geita yatakayofunguliwa Septemba 23 mwaka huu katika Halmashauri ya Mji wa Geita huku Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kufunga maonyesho hayo.

Akizungumza na waandisi wa habari katika viwanja vya EPZA vilivyopo katika Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema,maonyesho ya mwaka huu yamekuwa na mwitikio mkubwa kutokana na washiriki wengi Zaidi kujitokeza kuonyesha shughuli wanazozifanya.

“ Maonesho haya yalianza 2018 na mwaka huu ni maonyesho ya sita ya madini ambapo dhamira ni kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maarifa mapya watakayoyatumia katika shughuli za utafiti,kuongeza thamani na shughuli za uchenjuaji,

“Mwaka jana tulikuwa na washiriki 250 ,lakini mwaka huu washiriki walioingia mpaka sasa ni zaidi ya 400 maana yake mwitikio ni mkubwa na wananchi hasa wachimbaji wameelewa maana ya uchimbaji hususan makampuni yanayojihusisha na uchimbaji,uchenjuaji ,uongezaji thamani kwa maana kwamba wameona umuhimu wa kushiriki katika maonesho haya.”amesema Shigela

Aidha amesema,Mkoa umeweka mazingira mazuri ili kuwawezesha wadau wa sekta ya madini kuja na teknlojia mpya na rahisi zitakazowawezesha wachimbaji wadogo kufaidika na teknolojia hizo kwa kuwa na gharama ndogo za uchimbaji ,uchenjuaji na uongezaji thamani wa madini ili nchi ifikie hatua ya kuhifadhi dhahabu ambayo imeongezwa thamani kwa zaidi ya asilimia 100.

Mkuu wa Mkoa ametuamia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi hasa wanaojishughulisha na uchimbaji,uongezaji thamani na uchenjuaji wa madini kufika katika viwanja hivyo kwa lengo la kujifunza na kuonesha mitambo na mshine kwa ajili ya shugfhuli za uchimbaji.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania