DRC

Mwanajeshi Kutoka Jeshi ka Rwanda akamatwa na jeshi tiifu kwa serikali FARDC wakati wa mapigani wilayani Lubero Kivu Kaskazini mashariki mwa congo DRC

news image

Msemaji wa jeshi la Congo FARDC SOKOLA1 Kivu kaskazini kanali MAK HAZUKAY chini ya uongozi wa meja général BRONO MA NDEFU, wasema bwana IRADUNKUNDA Jean de Dieu kutoka jeshi la Rwanda alikamatwa wakati wa mapigano makali wilayani Lubero ,akihujiwa wakati wa mkutano na wanahabari Mjini Lubero Iradunkunda amesema amewa katika kikosi maamu cha jeshi la wananchi wa Rwanda na alizaliwaa katika Kijiji cha Ngororero eneo la Mulenge ,wilaya ya Kazadi alifanya mafunzo pa Liwawa kusini mwa Rwanda mwaka 2002,na kuingia DRC kupitia Mji wa KIBUMBA wilayani NYIRAGONGO KIVU KASKAZINI,mwajeshi huyu amesema mamae anaitwa Hakizimana Hamza na Kabayana Jacqueline.

IRADUNKUNDA JEAN DE DIEU, anasema ameshiriki katika operesheni kadhaa za kijeshi tangu uasi wa M23 kuendelea upande wa DRC ambako amepigana kwa muda mrefu na jeshi la Congo FARDC katika maeneo ya Rutshuru na kwa sasa LUBERO kwa mwaka mmoja na nusu.

IRADUNKUNDA JEAN DE DIEU alikamatwa baada yaku kujeruhiwa na kutibiwa kwa huduma ya kwanza na Huduma ya Afya ya jeshi laa Congo FARDC ,askari huyu amekuwa na silaha nizto na vifaa vingine vya kijeshi ambako alitumwa na viongozi wake DRC katika msako wa FDLR naku chimba madini katika misitu ya Congo kwa kukunufaika ,Irandukunda aomba wanajeshi wengine wa rwanda kuacha vita ambavyo vinanufaisha watu Fulani katika taifa la Rwanda vijana wengi wakipoteza maisha kwa udanganyifu ..

luteni Kanali MAK HAZUKAY amesema jeshi la Congo FARDC lina pambana kwakujibu mashambulizi na uchokozi na kwa sasa jeshi tiifu kwa serikali likiwa limerudi katika vijiji vya KASIKI, LUHANGA, na NDOLUMA operesheni zikiendelea katika eneo la MAMBASA na ALIMBONGO chini ya uongozi wa Meja Jenerali Bruno Mandevu, kamanda wa operesheni Sokola 1.

Germaine Hassan Kyahwere - AM/MTV News DRC