DRC

Muungano wa majeshi ya Uganda UPDF na Jeshi la CongoDRC FARDC watangaza kuwaokoa wananchi 90 wa mataifa mawili walio tekwa na kundi la kigaidi la ADF

SEPTEMBA 15, 2023
Border
news image

Muungano wa majeshi ya Uganda UPDF na Jeshi la CongoDRC FARDC watangaza kuwaokoa kwa mara nyingine wananchi 90 wa mataifa mawili walio tekwa na kundi la kigaidi la ADF hadi misituni Beni kivu kaskazini mashariki mwa Congo siku zilizo pita.

Akizungumuza na wanahabari toka vyombo vya Uganda na wale wa DRC katika Mji wa kasindi unao patikana mpakani mwa Drc na Uganda Général Dick OLUM kamanda wa jeshi la UPDF DRC asema Zaidi ya raia 90 wa Congo na Uganda waliokolewa katika mwezi mmoja wa operesheni kabambi katika misitu ya Beni ikiwemo wanawake 29 walio toroka kundi la kigaidi la ADF na washirika wao kwenye vijiji vya Ndalya kufuatia operesheni kubwa na suja za wana za muungano wa Uganda"Updf" na Kongo "Fardc".

"Opersheni inayo kuwa na lengo moja la kuhakikisha ADF inateketezwa , tangu hiyo opersheni ianze mwaka 2022 tume wauwa ,tume washika wengi zaidi , katika kushika ma ADF na katika hicho kitendo cha kuwa uwa n'a kuwa piga , ndiyo tuna okoa wanawake wengi na watoto , kuna wengine tunashika ambao ni wapiganaji .katika kuwashika Mara kwa Mara baada ya miezi huwa tuna waleta hasa wale ambao ni wakongomani tuna warudisha Kongo , Wale ambao ni waganda tuna warudisha Uganda umuhimu ni kwamba waungwe na familia Zao , kwa kuwa Mara nyingi wana shikwa kwa nguvu ama kushurutishwa kujiunga na ADF wengine wana danganywa "

Akisema Geberali Général Dick OLUM mkuu makamu wa operesheni sujaa eneo la Beni Kivu Kaskizini.

Utafahamu kwamba Uganda iliwaleta raia 22 wa Congo na wengine 8 wa Uganda .ADF inashutumiwa kuendesha vitendo vya uhalifu wa kivita na mauaji ya kinyama wilayani Beni na Mjini Beni Kivu kaskazini na sehemu moja ya Ituri wilayani Mambas ana wilayani Irumu.

Wananchi eneo hilo wakiomba jeshi la Uganda kupelekwa sehemu nyingine ambako waasi hao wa ADF wamekwenda kujificha akisema Saidi Balikwisha Mbunge wa Beni .Balikwisha ameomba wakaazi kuunga mkono operesheni hizo ambazo ndizo za tegemewa na raia wa eneo hilo ambao wanashuhudia mauaji tangu mwaka wa 2012 walipo anza kuwateka watu eneo la Mayimoja na Opera.

Ericksson Luhembwe -AM/MTVNEWS