DRC BENI

Muungano wa jeshi la Uganda UPDF na lile la Congo FRADC watangaza mafanikio makubwa katika opéresheni zao dhidi ya ADF wilayani Beni kivu kaskazini

AGOSTI 25, 2023
Border
news image

Muungano wa jeshi la Uganda UPDF na lile la Congo FRADC watangaza mafanikio makubwa katika opéresheni zao dhidi ya ADF wilayani Beni kivu kaskazini.

Akizungumuza na MTVNEWS MACK Hazukay msemaji wa Muungano wa opération za kijeshi za pamoja kati ya Uganda na DRC wilayani Beni na sehemu moja ya Ituri asema,kwasasa kuna mafanikio makubwa katika opéresheni za kijeshi kwenye bonde la Mualika ikiwa ni sehemu kubwa inayo kuwa katika mbuga la wanyama pori la Virunga na kukiwa muto mkubwa wa semuliki.

Hazukay ameongeza kwamba mbali na juhudi mbali mbali kuna vile doria za pamoja.

ADF inashutumiwa kuwaua raia wengi Beni kivu kaskazini na irumu mkoani Ituri kaskazini Mashariki mwa Congo , ADF ikiwa na makamanda wao kutoka Uganda na wakiunganisha mataifa mengi,kama Uganda,DRC, Tanzania, Soudan,kenya,Misumbiji na mataifa mengine ya kiarabu.

Kundi hilo likiwasajili watoto,vijana wanawake ambao hulazimisha kuwa wa Islam na kutii amari zao.maelfu ya watu wamepoteza maisha wilayani Beni tangu 2008 pale ADF ilipoanza kuwateka watu Mayimoya na oicha.

AM/MTV NEWS