DRC - BENI

Mradi wa maendeleo "wilaya 145" ume kamilisha kazi ya Ujenzi wa majengo 9 za shule na vituo vya afya 9 wilayani Beni

AGOSTI 16, 2023
Border
news image

Kila tarafa sekta na mitaa pame jengwa jengo moja la shule na kituo cha afya kimoja , vivyo hivyo katika mitaa na kufanya jumla ya shule 9 na vituo vya afya 9 kote wilayani Beni . Mkuu kiongozi wa wilaya ya Beni katika kipindi hiki cha mda wa dharura , kanali Charles Omeonga ana sema kuna miradi mingine zitakazo fuata , ikiwa pamoja na ukarabati wa barabara zitakazo elekea mashambani , umeme katika baadhi ya miji pia kupeleka maji safi palipo mahitaji , ila hakutoa tahere ambayo hawamu hiyo ya pili itaanza kutekelezwa.

Pamoja na hayo , kiongozi wa kirai wilayani Beni ana dhibitisha ujenzi wa shule na vituo vya afya , ila Bwana Richard KIRIMBA ana sikitika kuona kwamba thamani ya majengo hayo hai ambatane na kiasi cha Pesa zilizo pangwa (laki moja)kwa utekelezwaji wa mradi wa wilaya 145 . Ame pendekeza ku buniwe tume ya uchunguzi , ikayo chunguza kazi inayo endeshwa na iliyo kamilishwa , watakao kutwa na atia wapelekwe mahakamani . Kwa mjibu wa duru hiyo ni takriban asili mia 20 pekee iliyo timiziwa kwa jumla ya pesa zilizo tengwa minajili ya mradi huo.

Kiongozi wa mashirika ya kiraia wilayani Beni anasema hakuna Mradi wowote , kuhusu barabara umeme wala maji safi unao tekelezwa , ijapokuwa ndizo mahitaji zalizo pewa kipawa mbele katika mradi wa wilaya 145 anasema richard kirimba.

Wakati huo , katika jamii kuna isiya ya faraja sababu ya ujenzi wa majengo hayo , wengi wakisema watoto wata pata elimu katika mazingira mazuri . Baadhi ya vituo vilivyo jengwa kuna vilivyo teketezwa na waasi wanao zaniwa kuwa ADF na washirika wao.

Eriksson Luhembwe MTVDRC/BENI