TANZANIA

MKUU WA MKOA WA KIGOMA THOBIAS ANDENGENYE AITAKA MAHAKAMA KUU KUTOA HAKI KWA WANANCHI WANAOKOSA MSAADA WA KISHERIA

JANUARI 27, 2024
Border
news image

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la zimamoto Thobias Andengenye ameitaka mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma kuhakikisha inatoa Haki kwa Wananchi ambao wamekuwa wakikosa msaada wa kisheria.

Mhe. Andengenye amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki ya sheria ambapo amesema kumekuwa na changamoto kwa wananchi kukosa Haki zao kwa kukosa elimu ya masuala ya kisheria ikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa na mirathi.

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Kigoma Marick Marick amesema ili kutatua changamoto za upatikanaji wa haki kwa wananchi kahakama hiyo imeanzisha ushrikishwaji wa wadau wa sheria ikiwemo polisi na takukuru ili waweze kuwafikia wananchi kwenye utoaji wa elimu ya kisheria.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa dini Mkoani kigoma wamesema ili mwananchi apate haki watendaji wa mahakama hawana budi kuwa waadilifu kwenye utoaji wa haki.

MTV Tanzania