TANZANIA

Mkuu Wa Majeshi Akagua Nyumba 5000 Msomera

JANUARI 21, 2024
Border
news image

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba 5000 za makazi ya wananchi wanaohama kwa hiari yao kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kuja Msomea Handenj Tanga. Mradi huo unatekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)

Akikagua mradi huo, Jenerali Mkunda amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo n namna Vijana wa JKT wanavyoutekeleza mradi huo kwa weredi mkubwa.

Aidha ametoa rai kwa watendaji wote katika Mradi huo kuendelea kutekeleza mradi huo kwa uzalendo mkubwa.

Wakizungumza namna mradi huo ulivyo na unavyowaongezea maarifa na ujuzi utakaowasaidia kuutumia baada ya kumaliza mkataba wao na JKT. Baadhi ya Vijana wa JKT walikuwa na haya ya kusema

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania