TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

MEI 06, 2024
Border
news image

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika kikosi cha Jeshi 825 Mtabila iliyopo wilayani Kasulu mh Andengenye amesema kupitia mafunzo hayo jeshi linajivunia kuwa na jeshi la akiba imara na hodari na matunda ya kazi hiyo ni kuona taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu.

matunda ya kazi hiyo ni kuona taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu. Aidha andengenye amewaasa wahitimu hao kutokubali kulaghaiwa na kujiunga na vikundi mbalimbali vya kihalifu, kwani kukubali kulaghaiwa ni usaliti wa kiapo cha jeshi na usaliti kwa taifa ambalo limetumia gharama kubwa kuwaandaa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mkuu wa Tawi la Ugavi, Uchukuzi na Uhandisi Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Hawa Kodi amewataka vijana hao kutumia jukwaa hilo kuwaelimisha wengine kwa vitendo kuwa wao ni wazalendo na kujiepusha vitendo vitakavyowaingiza kwenye matatizo ya afya ya mwili na afya akili.

Naye, Muwakilishi wa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema kufuatia mafunzo hayo vijana hao watakuwa tayari kutumikia na kulilinda taifa popote watakapokuwa na kuwataka kutumia elimu waliyoipata katika kutatua changamoto mbalimbali pasipo kuvunja sheria, kanuni na taratibu za nchi.

AM/MTV DRC ONLINE .