DRC

Mizozo kati ya nchi wanachama na hali ya usalama mashariki mwa DRC kiini cha mazungumzo kati ya Felix Tshisekedi na ujumbe wa Bunge la CIRGL

AGOSTI 16, 2023
Border
news image

Ujumbe wa wana bunge wa "CIRGL" uli pokewa na raisi wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi juma Nne Ogasti 16 katika jengo la "Cité de l'Union africaine" katika Mji mkuu wa DRC , chini ya uongozi wake Bi Jemma Nunu Kumba ambaye pia ni msemaji wa Bunge la Sudan Kusini .

Akijibu kwa swali la waandishi habari Bi Kumba alisema " tumekuja DR.Congo kuonyesha ripoti iliyo chapishwa kwajili ya kusuhisha mizozo katika mataifa 4 wana chama ( Sudan Kusini , Soudan , Jamuhuri ya Afrika ya kati aidha Drc) . Tuli zungumzia pia mchakato wa Nairobi na Luanda" ali dhibitishia waandishi habari jijini Kinshasa Bi kumba .

Swala la hali ngumu kiusalama mashariki mwa DRC , ambako watu wengi wana hasirika na mizozo ya kivita , ni miongoni mwa mada zilizo kuwa kwenye meza ya mazungumzo katika mkutano huo wa kikanda , Msemaji wa Bunge la Sudan Kusini alisema .

Kama kumbukumbu ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu maeneo ya wilaya ya Rutshuru , Masisi , Nyiragongo na walikale mkowani Kivu kaskazini mashariki mwa DRC , kuvamiwa na majeshi ya Rwanda kwa ushiriki na kundi la M23 kwa mujibu wa serkali ya Kinshasa

Eriksson LUHEMBWE - MTVNEWS