KENYA

Mashauriano ya Serikali na Upinzani Kenya

AGOSTI 15, 2023
Border
news image

Cheche za maneno zinatarajiwa huku hoja kuhusu mazungumuzo ya maridhiano ikitarajiwa kuwasilishwa katika bunge la kitaifa nchini Kenya.

Hii ni baada ya kamati ya wanachama 10, ikiongozwa na kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa  Kimani Ichung'wah kukubaliana kuwasilisha hoja katika bunge la seneti na bunge la taifa kurasimisha mazungumzo hayo. kamati za kiufundi za mirengo yote miwili ya kisiasa  bado hazijaafikiana kuhusu ajenda za mazungumzo hayo.

Mrengo wa upinzani wa Azimio uko makini kuhakikisha wa gharama ya juu ya maisha na ukatili wa polisi dhidi ya waandamanaji yajumuishwe kwenye ajenda ya mazungumzo hayo, huku Mrengo wa Kenya Kwanza ukisisitiza kwamba masuala hayo hayatajadiliwa.Mazungumzo hayo yataendelea siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Dancan Maiche, Nairobi Kenya