DRC MASISI KIVU KASKAZINI

Mapigano Makali Yazuka Upya Kati ya Wapinganji Wazalendo na Waasi wa M23 Kaskazini Mashariki Mwa DRC

OKTOBA 04, 2023
Border
news image

Akizungumuza na idhaa hii Jules Mulumba kutoka makundi ya wazalendo asema kwa sasa hali ni ngumu na mapigano yaendelea kuwa makali kati ya waasi wa M23 na vijana wao wilayani masisi kwenye milima ya kilolirwe na milima jirani .mapigano hayo yalizuka tangu juma tatu na kwa sasa wakaazi wanao ishi kwenye vijiji husika wakikimbia makaazi yao kwa sasa wakiliekea katika Mji wa Kichanga na wengine Sake kaskazini mwa Mji wa Goma.

Mapigano inayo jiri wakati pande zote ziliombwa kuheshimu mikataba ya Burundi na Angola lakini wazalendo kwa uapande wao wakisema hawahusiki hata kidogo kwenye mikataba hiyo na watandelea kutwanga na M23 kwakilinda familia zao.M23 imekuwa ikomba mazungumuzo na serikali ya Kinshasa na Kinshasa ikisema haiwezekani kuzungumuza na M23 kwani ni sehemu ya jeshi la Rwanda linalo jitukuza kuwa waasi wa DRC.

DRC kwa sasa ina wanajeshi wengi kutoka Africa mashariki ,MONUSCO na hata SADEC ambao wote wamekuja DRC katika ulinzi wa amani lakini wote wakionekana kushindwa kutatua mzozo wa DRC kwani ni vita vya kisiasa na kiuchumi. Wakaazi wa mashariki mwa Congo wakishutumu mataifa ya Africa mashariki kuwa nyuma ya uasi wa kila siku wa mashariki mwa Congo japo wamefika kutaka tafuta suluhisho.

Wakaazi na mashirika ya kiraia ikomba serikali kufanya liwezalo kuhudumisha amani na usalama wa raia wambao wapitia hali ngumu na mbaya ya kimaisha katika kambi mbali zinazo zunguuka Mji wa Goma.

AM/MTVNEWS