DRC

Mapigano makali yaendelea kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali ya Congo DRC AFRDC

DISEMBA 11, 2024
Border
news image

Kwa mara nyingine mapigano makali imeshudiwa kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali FARDC katika Vijiji mbali mbali, ikiwemo Luofu magharibi mwa Mji wa Kaina, Kikuvo mashariki mwa Mji wa Kirumba na VUVOTSO karibu na Mji wa Kaseghe kusini mwa wilaya ya Lubero Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC.

Mapigano ambayo yana jiri siku moja ya utulivu, pande mbili zikipigana kwa zaidi ya wiki moja katika mji wa Kaseghe wilayani Lubero kwenye milima mirafu, mapigano yanayosababisha hali mbaya ya kiutu na wakaazi kushindwa kupata chakula na huduma ya afya. Serikali ya DRCongo ikiendelea kushutumu Rwanda kuendelea kuunga mkono waasi mashariki mwa Congo DRC wakati wako kwenye mchakato wa kutafuta amani na usalama Kanda ya maziwa makuu hasa mashariki mwa Congo.

Mapigano ambayo yaendelea katika uangalizi wa kikosi cha MONUSCO na kile kutoka kusini mwa Afrika SADEC ambao wote walikuja DRC kutafuta amani lakini wakigeuka kuwa waangalizi, wakitazama namna maelfu ya wakaazi waendelea kuhama vijiji vyao na kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kufariki dunia.

Umoja wa Mataifa MONUSCO umekuja Congo kulinda raia wa Congo lakini kwa sasa wakishutumiwa na sehemu kubwa ya wakaazi wa DRC kuwa waangalizi na kushindwa majukumu yao ambayo yanasababisha hali mbaya ya kiutu. Mapigano haya ya Lubero inajiri wakati marais wawili yaani Felix Tshisekedi wa DRC atarajia kukutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame nchini Angola chini ya usuluhishi wa Angola.

Wakaazi wa Congo DRC wakishudia machafuko kwa zaidi ya miaka thelathini kwa sasa katika uangalizi wa UN ambao wako DRC kwa zaidi ya miaka ishirini hadi sasa.

AM/MTV News DRC