TANZANIA

MAKAMU RAIS TANZANIA APINGA LUGHA ZA UVUNJIFU WA AMANI.

JANUARI 29, 2024
Border
news image

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Philipo Mpango Amewataka vijana kote nchini kuachana na matumizi ya lugha zenye viashiria vya uchochezi wa uvunjifu wa amani hasa wakati huu ambao Taifa linajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dkt.Mpango Ameyasema hayo leo Akiwa mkoani Kigoma wakati wa Kongamano la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutumiza miaka 3 madarakani pamoja na miaka 47 ya chama cha Mapinduzi Tangu kuanzishwa Kwake .

Mpango amesema wapo baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakitoa lugha zinazoashiria uchochezi kwa viongozi wa nchi huku akiwataka kuacha kufanya maandamano yasiyo na Tija na badala yake wajikite kufanya kazi ili kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla.

Tryphone-MTV Tanzania