DRC - GOMA

Mahakama Ya Kijeshi Ya Wapa Ya Wahukumu Wanajeshi Walio Husika Katika Mauaji Ya Waandamanaji Goma

OKTOBA 03, 2023
Border
news image

Mario Ngavo Mkuu kiongozi wa shirika za kiraia Mjini Goma asema mahakama imefanya kazi nzuri kuwahukumu wanajeshi walio husika na mauaji ya waandamanaji kutoka kanisa la wazalendo walio kuwa wakiandaa maandamano tarehe thelathini Agosti ilio pita ,kesi hii imesikilizwa kwa Zaidi ya wiki tatu hadi sasa ,mahakma ikiwapa adhabu mbali mbali wahusika na kuwachilia wa wili miongoni mwao hasa Luteni kanali Bawili ,huku Mike Mikombe akihukumiwa kifo na kufukuzwa katika jeshi kwa makosa ya kutekeleza mauaji kimakusudi na kutumia vibaya jeshi na risasi za serikali.

Serge Lukanga wakili wa Mikombe amsema ataka rufaa kwani mteja wake hakutendewa haki .hatua hiyo vilevile ikichukuliwa na upande wa raia nao wakijipanga kukata rufaa kwani hawaja tendewa haki hasa kuwalipa ndugu zao walio uwawa na serikali,Edmond mmoja wa familia amesema kuhukumu Mike mikombe ni vizuri ila ingekuwa muhimu kuwakamata walio muruhusu mikombe kuwawa raia kwani Kivu Kakaskazini kuna Kambanda wa Operesheni.

Espoire Aspirini kutoka kundi la Vijana wa Lucha akiomba wahumini wote kutoka wazalendo walio kamatwa kuachiliwa kwani hawana kosa lolote akisisitiza.huku mahakama ikimuhukumu Ephrem mkuu wa baraza la wazalendo.

AM/MTVNEWS