DRC - BENI

Generali Muhanga Kutoka jeshi la UPDF aomba raia kuwaunga mkono katika opéresheni za kijeshi zidi ya ADF mwalika wilayani Beni

AGOSTI 16, 2023
Border
news image

aki himiza wakongomani kwa vita inayo endelea Bondeni Muhalika wilayani Beni.Hii Ogasti 16 , 2023 Muhanga aomba Raia waishio mkowani Kivu kaskazini hususan wilayani Beni , maeneo ya karuruma , kijijini kalibuli , wame pongeza opersheni inayo endeshwa na Jeshi la Uganda "UPDF" , général Kayanja Muhanga Ali toa pia shukruni zake kwa Rais na kiongozi mkuu wa majeshi ya Uganda Yoweri kaguta na mwenziwe wa DRC Felix Tshisekedi kwa kutumika pamoja ili kutokomeza magaidi wa kundi la " alliance Democratic forces " ADF .

Wachambuzi mbali mbali wame dai kwamba operesheni Shujaa ime leta mabadiliko kwa kiwango fulani katika wilaya ya Beni , mkufunzi Muse kakule amesema

" Maendeleo haiwezekani bila amani , kwa amani inayo onekana kwa sasa barabara zina weza kujengwa. tuna tumika katika mtandao wa barabara Beni -Butembo kwa kuendesha shughuli za kibiashara na zile za kimaendeleo . Shukrani zetu kwa majeshi ya muungano Fardc updf walio raisisha hivi "

Bwana Matara Tembeya , muwakilishi wa Mkuu kiongozi wa wilaya ya Beni mjini karuruma , alihimiza raia wote kuunga mkono operesheni Shujaa ili amani ya kudumu irudi jimboni . " Fardc na Updf wana hitaji ya uungwaji mkono wetu , tuwa pongezi wame chapa kazi nzuri . Yafaa tuungane ili kufukuza magaidi katika maeneo yetu "

Luteni Generali muhanga alitoa shukurani zake kwa wananchi kwa ukaribu wao unao wezesha muungano wa majeshi kumu shinda Adui ADF mkowani Ituri , hasa zaidi tarafani Tshabi , maeneo ya Kainama , kambi ya Jua , tarafani Boga , Malibongo , zunguluka na Malulu .

" Sasa nguvu zetu zote zime elekezwa kule bondeni Muhalika , tuna hitaji ushirika wenu kwa kiwango cha juu kabisa ili kumtokomeza adui ADF na kumfukuza mbali "

alisema luteni Generali muhanga .

Bonde la Muhalika , hapo mbeleni lilikuwa ni ngome ya ADF , kwa ku pokea watu kutoka sehemu mbalimbali, kwajili ya mafunzo ya makurutu , chini ya uangalizi wa Makanda wa ADF kama Amigo na Mulaalo . Mulaalo ameisha uawa na majeshi ya muungano mwanzoni mwa mwaka huu 2023 , ila Amigo ameisha ponyoka mara kadhaa chupuchupu , katika mashambulizi kadhaa . Majeshi ya muungano yame fanya jitihada kuhakikisha magaidi hawako tena katika bonde la Muhalika .

Luteni Generali muhanga , aki sindikizwa na Meja jenerali Dick Olum , kamanda mkuu wa operesheni Shujaa na Makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Fardc mkowani Kivu kaskazini , kama kanali Gilbert Bakavuo , kamanda wa operesheni "sukula1" jimboni Beni , kanali Munanga , muratibu wa operesheni Shujaa , kanali Makela , kamanda wa sekta 3 , kanali Rizza Ibazza . Wote pamoja wali tembelea vikosi na Makanda mbalimbali .

Major Bilal Katamba
Afisa wa habari
Kikosi cha milimani /opersheni Shujaa.

MTVNEWS