TANZANIA

Kufunguliwa kwa Kituo cha Polisi Mbande Dar es Salaam Tanzania kumesogeza huduma za kipolisi kwa wananchi Kata ya Chamazi

SEPTEMBA 2, 2023
Border
news image

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Tanzania SACP. Muliro J. Muliro amezindua jengo la kituo cha Polisi Mbande, kilichopo Kata ya Chamazi, Mbagala Jijini Dar es Salaam ambapo awewataka askari kukifanya kituo hicho kuwa msaada kwa wananchi katika kuzuia na kudhibiti uhalifu na kuwa kimbilio la haki katika kutoa huduma za kipolisi.

SACP. Muliro amesema kituo hicho kioneshe matokeo makubwa ya kuzuia uhalifu ili tofauti iweze kuonekana harika kabla na baada ya kujengwa kituo hicho "Mkuu wa kituo uliopangwa kufanya kazi hapa na askari, mfanye kazi kwa kushirikana na wananchi li utulivu ongezeke katika maneo haya ya Chamazi na mitaa yake." SACP Muliro alisema

Katika hatua nyingine amewakumbusha wananchi umuhimu wa kutoa ushahidi mahakamani kwani ushaidi wa Polisi pekee hauwezi kusababisha mtuhumiwa kukutwa na hatia, kwa kutofanya hivyo watuhumiwa watakuwa wanaachiwa huru kwa kukosekana kwa ushaidi wa walalamikaji mahakamani.

Ujenzi wa kituo hicho cha Polisi Cha Daraja B unakadiriwa kufika milioni 100, akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ACP. Kungu Malulu amesema kituo hicho ulianza mwaka 2016 na kimejengwa na Polisi kwa kushirikiana, na wananchi na wadau wa masuala ya kiusalama na kukamilika kwa ujezi huo, kumeleta huduma za kipolisi karibu zaidi na wananchi tofauti na ilivyo kuwa awali.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Chamazi Injinia John Gama amesema askari wasiwafanye wananchi walioshiriki katika kukijenga kituo hicho wanung’unike kwa kukosa haki pia amewakumbusha wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika kufichua wahalifu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Awadhi Hemedi amewataka wananchi kotogopa kufichua wahalifu kwani kunapokuwa na wahalifu amani hakuna na pasipo na amani maendeleo hakuna.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania