KENYA

Kongamano la bara la Afrika kuhusu maswala ya hali ya hewa litakuwa likifanywa kila baada ya miaka miwili na kuandaliwa na mataifa wanachama wa muungano wa Afrika ili kuimarisha ruwaza mpya ya bara hili

SEPTEMBA 6, 2023
Border
news image

Kongamano la bara la Afrika kuhusu maswala ya hali ya hewa litakuwa likifanywa kila baada ya miaka miwili na kuandaliwa na mataifa wanachama wa muungano wa Afrika ili kuimarisha ruwaza mpya ya bara hili.

Hayo yametangazwa na mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Mousa Faki kama sehemu ya maamuzi yaliyofikiwa huku kongamano la siku tatu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ukikamilika rasmi hii leo.

Rais William Ruto alisema kuwa ushirikiano mkubwa wa mataifa ya bara la Afrika ulioshuhudiwa wakati wa kongamano hilo, ulidhihirisha kuwa bara la Afrika limechukua mwelekeo ufaao huku akiongeza kuwa kuwa ushiriki wa nchi za Afrika katika kongamano hilo umekuwa wa kupigiwa mfano.Wadau mbalimbali wa maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa walipata fursa ya kuangazia suluhu zinazohitajika kushughulikiwa huku mjadala kuhusu maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa ukiendelea kushika kasi. Watoto na vijana wa bara la Afrika wanataka kujumuishwa katika mchakato huo.

Kongamano hilo la bara la Afrika kuhusu maswala ya hali ya hewa lilihudhuriwa na marais 17 kutoka mataifa ya bara la Afrika na kuwavutia zaidi ya wajumbe elfu 30.

AM/MTVNEWS