Kuelekea ziara ya mbio za mwenge 2023 katika mkoa wa Kigoma,Wilaya ya Kigoma imejipanga kuhakikisha miradi yote 11 yenye thamani ya shilingi 5.5 bilioni inazinduliwa.
Akizungumza leo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Hamis Kali amesema miradi hiyo imetekelezwa kwa fedha za ndani na fedha za wahisani.
Kali ameitaja baadhi ya miradi kuwa ni pamoja na ugawaji wa pikipiki kwa watendaji wa kata,zahanati mbili,masoko mawili,vumba vya madarasa vilivyojengwa kwa fedha za ndani,miradi ya uhifadhi ya mazingira.
Mratibu wa mwenge Halimashauri ya wilaya ya Kigoma Innocent Mdunya amesema mwaka huu hawatarudia makosa ya mwaka jana ya baadhi ya miradi kukataliwa na mwenge kwani wamekuwa wakifanya ufuatiliaji mkubwa na wakaribu ili miradi yote ikidhi vigezo.
Mwenge wa uhuru unatarajia kuwasili mkoani Kigoma Agost 18 katika Wilaya ya Kakonko na Agost 20 utawasili katika Wilaya ya Kigoma ukiongozwa na kauli mbiu,"Tunza mazingira,okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa taifa".