TANZANIA

Kero za Wananchi katika Maeneo Yetu Tanzania, Zitatatuliwa Nasisi Wenyewe - Kikwete

SEPTEMBA 4, 2023
Border
news image

Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiongea na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Halmashauri Wilayani hapo.

Akizungumza katika mkutano huo, Ndg. Ridhiwani amewakumbusha madiwani kuwa mbele katika kutatua kero za wananchi na sio kusubiri viongozi wanaowaita “wa juu” ili waende kutatua kero katika maeneo yao.

"Aliwaasa wajumbe kushughulikia kero za wananchi katika maeneo yao pale zinapotokea bila kupoteza muda".

Katika mkutano huo pia, Ndg. Mawazo Mkufya alichaguliwa kwa kura 19 kati ya 21 zilizopigwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja na kamati za madiwani pia ziliundwa upya na kupata viongozi pia.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania