TANZANIA

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM DKT EMMANUEL NCHIMBI AOMBA VIJANA WA CCM KUWA IMARA

news image

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Chama CCM Itaendelea kuhakikisha vijana wa chama hicho wanaandaliwa kwa weledi na kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama na Serikali ili kusaidia wananchi, na kuagiza Vijana kuacha kuwa na mpasuko kwa madai ya kutaka uongozi.

Mheshimiwa Nchimbi amesema hayo katika hotuba ambayo imesomwa kwa niaba yake na mkuu wa idara wa organaizesheni wa chama hicho Issa Haji Gavu baada ya wajunbe wa baraza kuu kukagua miradi ya maendeleo na kufanya tathmini ya UVCCM ambapo amesema wanatakiwa kudumisha mshikamano na umoja ndani ya chama.

“hakuna yeyote atakayetoka nje kuja kuchukua nafasi ndani ya ccm kama hakupittia kwa vijana na wa uvccm ili awe ameiva kutokana na mafunzo tunayowapa vijana wetu na kuwaanda kuwa jasiri na weledi kwa utumishi”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka vijana kutojiingiza katika matendo maovu na badala yake kusaidia katika utatuzi wa changamoto za wananchi ambazo zinawakabili ili huduma zitolewee kwenye jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa UVCCM Taifa Mohamed Kawaida ameeleza kuwa jumuia hiyo ya ccm itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana ili waweze kutumia fursa zilizopo ndani ya chama na nje ili kuwa na taifa lenye hazima kubwa kwenye siasa na uongozi.

Tryphone Odace - MTV Tanzania