DRC

Jeshi la taifa la Congo FARDC limetangaza kuzima maandamano na vurugu zilizo pangwa na wahumini wa kanisa Moja la wazalendo

AGOSTI 30, 2023
Border
news image

Akizungumza na sauti ya America kwenye kata la ndosho magharibi mwa Mji wa Goma Luteni Kanali Ndjike ameomba wakaazi wa Mji wa Goma kuwa waangalifu kwani jeshi halita vumilia mutu yeyote atakae yumbisha usalama .

Ndjike ameongeza kwamba jeshi limefanikiwa kuzima maandamano ya vurugu ulio andaliwa na wahumini wa kanisa ya wazalendo na watu saba wamefariki Dunia,Zaidi ya ishirini kujeruhiwa na wengine Zaidi ya miamoja hamsini kukamatwa.

Wahumini wa kanisa hilo la wazalendo wakisema hawatakubali vitisho kutoka kwa wanajeshi kwani wanapigania uhuru wao.Polepole Buhendwa Mbafumoja ni mmoja wa wahumini hao asema hawata tishika japo wanaandamwa na vyombo vya usalama.

wahumini hao wakiwa wametawanyika na zehebu yao kuchomwa moto.Msako ambao umepelekea shughuli kufungwa katika Mji wa Goma na kuzusha wasiwasi miongoni mwa raia .ila jeshi likiomba wananchi kuwa watulivu.

Kwa saa za jioni shughuli zimerudi kawaida kwa sehemu ndogo katika Mji wa Goma baada ya operesheni kabambi za jeshi la Congo Fardc kuzima maandamano hayo na kuwakamata wahumini wa kanisa la wazalendo Pamoja na kanisa lao kuchomwa moto.

AM/MTVNEWS