DRC

Jeshi la serikali ya Congo latangaza kumkamata mbunge wa zamani wakati wa mapigano kati ya ADF na Muungano wa jeshi la FARDC na UPDF.

Aprili 26, 2024
Border
news image

Akizungumuza na vyombo vya Habari Mjini Beni Antony Mwalushayi msemaji wa jeshi eneo husika asema jeshi la Congo FARDC likiungana na lile la Uganda UPDF limewaua wapiganaji tano wa kundi la ADF na kuwakamata wengine katika Kijiji cha Ngite karibu na Mji wa Mavivi unao patikana karibu na uwanja wa Ndege wa Beni.

Mwalushayi akiwa Msemaji wa operesheni za kijeshi amesema Mbunge Ngahangondi anae julikana sana na wakaazi wa Beni na ambae alikuwa Mbunge kivu Kaskazini alikamatwa na jeshi wakati wa operesheni kali ya msako wa wapiganaji wa ADF ambao waliingia kwenye mtego.kwa mjibu wa Ngahangondi ni kwamba mwenyewe aliingia katika eneo hilo bila kufahamu kuna nini kwani alikuwa akitembeza pikipiki kwa saa za jioni akitoka Mjini Beni ambako kuna ofisi yake ya kazi. Ngahangondi anasema hajaelewa kwa nini Msemaji wa jeshi kutangaza kwamba yeye alishirikiana na waasi japo yeye alinusurika kifu ,na kuwa ilikuwa amejificha ndio baadae kaona gari za kijeshi nakuomba msaada wa uokozi ndio akabebwa moja kwa moja na kupelekwa kwenye kituo cha jeshi. Ngahangondi aliongeza kwamba hajawai kushirikiana na ADF na haiwezenake kushirikiana na ADF ila kila siku amekuwa ikishutumu watu Fulani kwenye vyombo vya usalama kushirikina na ADF nah ii huwa ndio sababu ya kumshutumu kuwa yeye anashirikiana na ADF. Msemaji wa jeshi eneo la Beni alisema Ngahangondi iliitishwa na vyombo vya usalama siku zilizo pita na kuwa atahaojiwa Zaidi kuhusu kupatikanae neo la waasi wakati wa mapigano . Utafahamu kwamba Ngahangondi amekuwa na makaazi yake katika Mji wa Oicha na ofisi zake Mjini Beni na kila asubui kama jioni hutoka oicha hadi Beni na Beni hadi OICHA. Laliki kwa sasa akiwa mikoni mwa jeshi .

AM/MTV DRC ONLINE