DRC

Jeshi laa Congo FRADC lajibu mashambulizi ya waasi wa M23 baada ya kuchukuwa Mji wa Sake ulieko magharibi mwa mji wa Goma

JANUARI 23, 2024
Border
news image

Jeshi la serikali ya Congo FARDC lime pambana vikali na waasi wa M23 katika eneo la Kasengezi karibu na Mubambiro baada ya waasi hao kushambulia Mji wa Sake ulieko wilayani Masisi ukiwa hata hivyo karibu na Mji wa Goma.

Waasi wa M23 wamechukuwa sehemu kubwa Kivu Kaskazini, serikali ya Congo DRC ikisema waasi hao wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda kwa uvaamizi wa ardhi ya DRC ndio sababu kubwa na vita mashariki mwa Congo ambavyo ni vita vya kiuchumi na uvaamizi wa ardhi wasema wachambuzi.

Shambulizi la leo la Mji wa Sake upatikanao kwenye kilometa zaidi ya ishirini magharibi mwa Mji wa Goma ni pigo kubwa kwa serikali ya Kinshasa na iwapo Mji huo utachukuliwa ama kutekwa na waasi wa M23 itakuwa haibu kwa Umoja wa Mataifa na vikosi vya SADC ambavyo vimekuja DRC kwa ajili ya kuungana na serikali ya Congo kulinda usalama wa taifa hili.

Kushambuliwa kwa Mji wa Sake kuna hasara kubwa kwa wakimbizi wanao patikana karibu na kambi za Mugunga, Bulengo na Lushagala ambazo zipo karibu na kambi za wakimbizi.

Vikosi vya MONUSCO na SADC kwa mara ya kwanza vimeonekena kusimama imara kwa ajili ya ulinzi wa Mji wa Goma. Taarifa zasema askari mmoja wa Afrika Kusini alijeruhiwa na baadhi ya wanawake wa wanajeshi walifariki dunia wakati wa shambulizi wa kambi ya jeshi saa za usiku.

Mji wa Goma ni mji muhimu kwa Kivu Kaskazini na mji ambao ni muhimu kwa eneo nzima la mashariki ya Congo na kanda ya maziwa makuu.

AM/MTV News DRC