DRC

Jamii ya Watwa Jimboni Tanganyika Yadai Kubaguliwa

SEPTEMBA 13, 2023
Border
news image

Katika Kijiji Cha kaminonge Takribani 30km kutoka Kalemie. Raia wa jamii ya watwa wamesema ubaguzi na Unyanyasaji dhidi Yao unawasababisha kukosa furaha ya kuwa karibu na wabantu.

Raia hao waliopo katika Kijiji Chao kidogo wamedai kunyanyapaliwa na raia wabantu Kwa kutupiwa maneno ya kejeli

Wakiwa wanahitaji maridhiano na mshikamano Ili kujenga Congo iliyo na upendo, upande wao wanadai kushangazwa na tabia za wabantu ambao wanawatupia maneno ya ubaguzi ya ukabila kwakudai wao ni chafu

Baadhi ya raia hao walituambia hata wanapotaka kuomba Maji ya kunwa wakiwa wanapita wanazarauliwa na kupewa Maji kwenye kikombo kichafu

Hata hivyo, raia hao wameiomba serikali kutambua uwepo wao katika jamii kuna faida kubwa licha ya wabantu kudai wao ni wanyang'anyi na waporaji jambo ambalo wanakanusha wakidai sio Kila mtu anatekeleza vitendo hivyo

Upande wa serikali kupitia mkuu wa maswala ya Kijamii jimboni Tanganyika YEMBA WA YEMBA ISDOR amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka sehemu mbalimbali jimboni Tanganyika.

Afisa huyo aliongeza kuwa jamii husika zinatakiwa kujiepusha naubaguzi unaoweza kusababisha vita ya kikabila jimboni Tanganyika

Ikumbukwe kuwa Jimbo la Tanganyika ni miongoni mwa majimbo nchini humu DR Congo yanayopitia vita ya kikabila mara kwa mara.

Zuberi Ally