KENYA

Helikopta Ya Jeshi La Kenya Yaanguka Lamu, Idadi Isiyojulikana Ya Wanajeshi Wafariki

SEPTEMBA 19, 2023
Border
news image

Helikopta ya Jeshi la Anga la Kenya imeanguka kaunti ya Lamu kaskazini mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu wakiwemo wanajeshi.

Kikosi cha Ulinzi cha Kenya katika taarifa leo Jumanne kimesema kuwa Helikopta ya Jeshi la Wanahewa la Kenya aina ya Huey ilianguka Jumatatu usiku ikiwa katika doria ya usiku katika kaunti ya Lamu.

"Wahudumu na wanajeshi wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa sehemu ya kikosi cha waangalizi wa anga kikiimarisha doria za mchana na usiku na ufuatiliaji wa operesheni inayoendelea Amani Boni," KDF ilisema katika taarifa.

"Uongozi na udugu wote wa KDF wanafariji familia za wafanyakazi."

KDF pia ilibainisha kuwa bodi ya uchunguzi imeundwa na kutumwa katika eneo la tukio ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na KDF kwenye mitandao yao ya kijamii, walisema kuwa helikopta hiyo ilikuwa na wafanyakazi na wanajeshi wengine ndani ya ndege hiyo.

Dennis Chisaka - Nairobi,Kenya