TANZANIA

Hatutokuwa Na Huruma Na Wanaowaonea Wanyonge Tanzania - Kikwete

SEPTEMBA 12, 2023
Border
news image

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Mhe.Ridhiwani Kikwete amewaagiza watumishi wa umma kuzinagatia sheria na kanuni za kazi zao katika kuwahudumia wananchi huku akisisitiza kuwa waaminifu.

Mhe.Kikwete ameyabainisha hayo kwenye ziara yake Mkoa wa Mara ambayo anatembelea miradi mbalimbali ya serikali na kuingea na watumishi wa Manispaa ya Musoma na kisha kufanya ziara kukagua utekelezaji wa mpango wa kuondoa Umaskini yaani TASAF katika mkoa huo wa Mara.

Naibu Waziri Kikwete ambaye annafanya ziara ya siku tatu katika Mkoa huo aliwaelekeza watumishi wa Umma kujikita katika kuhakikisha wanazingatia na kutafsiri maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan nakuwahimiza kuwa na Utumishi wenye kuleta tija, ubora, ulio na mkakati unaolenga kuwatumikia wateja ambao ni wananchi bila ubaguzi.

Akizungumza na watumishi Naibu Waziri hiyo aliwaasa kuwa wabunifu na wenye mikakati inayotekelezeka ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Katika hatua nyingine Naibu waziri Kikwete amewaondoa kwenye nafasi za uratibu wa mpango wa TASAF waratibu wa Mkoa huo na Wale wa Wilaya kwa kile alichisema wameshindwa kufikia malengo ya kuwahudumia na kuwafikia wananchi wanyonge kwa wakati ambao wanauhitaji na huduma hiyo kwasasa.

Akionyesha kukasirishwa na kitendo hicho cha waratibu kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo Mhe.Kikwete alimuuliza RAS wa Mkoa wa Mara ndugu Makungu "kwanini hadi leo wahitaji hao hawajalipwa wakati fedha kwa ajili ya wanufaika zilishatumwa nakuelekezwa wakalipwe wanufaika hao ambao ni kaya maskini?" aliuliza

Naibu Waziri anaendelea na ziara yake Mkoani Mara kwa kuelekea Wilayani Tarime ambapo atazungumza na watumishi na kutembelea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kwa wakati.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania