DRC MANGINA

Hali ya usalama yaendelea kuwa ya wasi wasikatika Mji wa Mangina wilayani Beni Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo kutokana na mashambulizi kutoka watu wanao dhaniwa kuwa ADF

APRILI 19, 2024
Border
news image

Akizungumuza na Channel Africa kwa Njia ya simu masaa machache baada ya watu wanao dhaniwa kuwa ADF kushambulia Mji wa Mangina Mangodomu Reagen Duchuma Kiongozi wa Vijana asema kwa sasa hali ni ya wasiwasi baada ya mashambulizi ya makaazi na vituo vya afia katika mji wa Mangina kata la Mangodomu.

Wakaazi Wakishutumu wapiganaji wa adf ambao kwa saa za usiku waliingia katika Mji wa Mangina na kuwawa watu wa wili na pikipiki zao kuchomwa moto na wengine kutekwa .Duchuma ameomba vijana kushirikiana na jeshi tiifu kwa serikali.

Mumbere Syavuli Sembo mkaazi wa Lubero asema mauaji ya Beni inaendelea kuwashangaza watu wengi hasa wakaazi wa Beni ,Lubero na sehemu moja ya Ituri Kuhusiana na mashambulizi ya ADF akisema Hubert Masomeko mtafiti na Mchambuzi wa maswala ya maziwa makuu hasa mashariki mwa Congo.

Katika mwezi mmoja watu Zaidi ya samani wameuwawa wote wakiwa mashambani na wengine wakiwa nyumbani kwao Mjini Beni vijiji vya Buruchu,Bunzi,Mapemba na mangina.

Hii katika uangalizi wa Kikosi cha Umoja wa mataifa MONUSCO na jeshi tiifu kwa serikali ya Congo FARD.

AM/MTV DRC ONLINE