DRC

Hali imerudi tulivu Mjini Goma baada ya maandamano na vurugu toka kwa wanafunzi kukemea kampuni za mitanda wakiomba mwanachuo aliye tekwa aachishwe huru

news image

Hali imerudi tulivu Mjini Goma baada ya maandamano n'a vurugu toka kwa wanafunzi kukemea kampuni za mitanda wakiomba mwanachuo aliye tekwa aachishwe huru

Hali hiyo ilishuhudiwa alhamisi majira ya asubuhi Ogasti 17, katika baadhi ya barabara jijini Goma mji mkuu wa mkowani wa Kivu kaskazini.

Hali ambayo inafuatia kisa cha utekwaji wa mwanachuo, anaye somea kunako chuo kiitwacho "ISTA", aliye tekwa tangu Ogasti 14 jijini Goma. Watekaji wana omba fidia ya dolla za kimarekani 10.000 ili kumwachia uhuru wake, kamati ya wanachuo wa Congo wame toa mwito kwa wanafunzi toka vyuo na vyuo vikuu kuwa katika umoja katika tukio hili, huku kamati hilo liki tahazarisha viongozi wa jiji la Goma kuwa tayari kwa chochote kile endapo mwenzi wao hata achiwa uhuru wake.


Hali ilirudi tulivu majira ya mchana pande ya saa 7 mabarabarani jijini Goma, vitendo vya utekwaji vimekuwa viki shuhudiwa mara kwa mara jijini Goma. Hali hii ime jitokeza tena baada ya utulivu wa kipindi cha miezi miwili, mvulana mwengine anaye fahamika kwa jina la Fabrice Kamwanya pia muhubiri alitekwa Ogasti 14, hadi sasa hatma yake haijulikane imesema familia yake, Bunge la vijana mkowani Kivu kaskazini laomba viongozi kuingilia kati kabla makubwa kuliko hayo haya jatokea.

Aline Kataliko, Erickson Luhembwe