DRC

Goma DRC kazi za ujenzi wa soko kuu ya kisoko katoyi zaanza Rasmi Mjini Goma.

MEI 06, 2024
Border
news image

Gavana wa Kivu kaskazini Peter Cirimwami akiandamana na kamati ya usalama wa mkoa wa Kivu kaskazini ameweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko kuu ya Katoyi inayo julikama kama kisoko.Mradi ambao unapongezwa na wananchi wa eneo huzika.

Peter Cirimwami alisema hii nikatika mipango ya rais wa Congo katika ujenzi maendeleo wa taifa japo vita vinavyoendelea mashariki mwa DRC kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 ambao serikali yasema wanaungwa mkoni na Rwanda. Kiongozi wa kata asema hii ni ishara kubwa kuona serikali imekumba wakaazi wake ambao walikuwa wakiendesha bishara yao pembeni ya barabara wakiwa na hatari ya kugongwa na gari ama pikipiki lakini soko hiyo itasaidia watu wote kuwa na nafasi nzuri sokoni.

Ujenzi huu unakuja wakati Mji wa Goma wakaazi wake wapitia hali ngumu ya maisha,ukosefu wa usalama,na wakimbizi wakiwa wengi mno kutokana na vita vya M23 ambayo serikali ya DRC inasema ni taifa la rwanda linalo endesha vita mashariki mwa Congo katika kila wanaita wizi wa madini.lakinki Rwanda ikisema nikutokana na Usalama wa taifa lake.

AM/MTV DRC ONLINE .