DRC

Gavana Mpya wa Kijeshi Kivu Kaskazini Aomba Wapiganaji wa M23 Kusalimisha Silaha na Kujiunga katika Mchakato wa Amania wa PDDRCS

SEPTEMBA 23, 2023
Border
news image

Piter Cirimwami Gavana mpya na wa Muda wa kijeshi Kivu kaskazini mashariki mwa Congo aomba wapiganaji wa M23 ambao ni raia wa Congo kusalimisha silaha zao kwa serikali na kujiunga na mpango wa PDDRCS mpanga ambao ulikubaliwa na ma Rais wakati wa Mkutano wa Angola ulio pelekea pande zote kusimamisha mapigano lakini M23 ikisema haipo kwa mpango huo kwani wanacho hitaji ni mazungumuzo ya moja kwa moja na serikali ya Kinshasa.

Mapiganao kati ya M23 na jeshi la serikali imesabisha wakaazi wengi kuhama vijiji,na makaazi yao wilayani Rutshuru,Masisi,na Nyiragongo na uongozi wa serikali kupoteza eneo zao.Gavana Mpya wa kijeshi ametembelea Mju wa musahaki unao patikana wilayani Masisi kaskazini magharibi mwa Mji wa Goma.eneo hilo likiwa chini ya uongozi wa kikosi kutoka Africa mashariki EAC hasa kikosi kutoka Taifa la Burundi.

Piter Cirimwami amesema ni sheriti watu wote kushiriki Uchaguzi ndio sababu eneo zote lazima zirudi katika uongozi wa serikali ya Kinshasa .kinshasa ikisema haiwezi kuzungumuza na M23 na M23 ikisema lazima izungumuze na Serikali .wanao hathirika katika kutoleweana ikiwa ni wananchi.

Akiwa Marekani Rais wa Congo Felix Tshisekedi amsema hakuna Mazungumuzo na M23 itakayo fanyika.

AM/MTVNEWS