DRC Kivu Kaskazini

Gavana mpya wa kijeshi ameomba jeshi tiifu kwa serikali kuendelea kuheshimu mikataba ya usitishwaji wa mapigano, wakiwa makini kutokana na uchokozi wa M23

SEPTEMBA 27, 2023
Border
news image

Nibaada ya kikao cha kamati ya usalama kufanyika hii juma tatu kunako ofisi ya gavana Mjini Goma ndipo hatua ya kamati ya usalama anayo ongoza Gavana wa Mkoa huoMeja Generali Piter Cirimwami Kuba imeamua kuendelea kuheshimu mikataba ya usitishwaji wa Mapigano ilio wekwa Angola na Burundi .kamati hiyo hata hivyo imeomba wanajeshi walieko kwenye mustari wa Mbele wa mapigano kuwa makini kutokana na wasiwasi ya waasi wa M23 ambao wameanza kurudi katika eneo walizo ziacha tangu usitishwaji wa mapigano.

Meja Generali Chirimwami gavana kwa muda Kivu Kaskazini alimgomboa mwenzie Constant Ndima baada ya vyombo vya usalama kuwaua raia wasio na hatia Zaidi ya hamsini tarehe thelathini ilio pita na wengine kadhaa kujeruhiwa na hata wengine kukamatwa na kuwekwa gerezani ambako wapatikana kwa sasa wakisikilizwa na mahakama ya kijeshi.

Wananchi wa Kivu Kaskazini wakiomba gavana Huyo kuwaletea usalama kuliko kubaki ofisini kwani wanancho kihitaji nikuona miji na eneo zote zina rudi Pamoja kabla ya uchaguzi kufanyika.tangu alipo teuliwa kama Gavana Kivu kaskazini gavana alitembelea mustari wa mbele wa mapigano na kuzusha hali ya wasiwasi katika uongozi wa M23 .M23 kwa upande wao wakiendelea kuomba mazungumuzo lakini serikali ya Kinshasa ikisema mazungumuzo hayo hayata kubalika .

Serikali ya CongoDRC inashutumu Rwanda kuunga mkono Kundi la waasi wa M23 ,lakini Rwanda ikikanusha kwa mara kadhaa uungwaji mkono ,taasisi mbali mbali ikiwemo serikali za Ulaya na Marekani ikisema kuna ushuhuda Tosha kuhusu uasi huo kuungwa mkono na Taifa Jirani la Rwanda.

Uasi wa M23 umesababisha mgawanyiko mkubwa kati ya DRC na Rwanda na baadhi ya mikataba kati ya mataifa hayo kuvunjika hasa ya biashara ya madini.

AM/MTVNEWS