DRC

Gavana kwa muda wa Kivu Kaskazini EKUKA LIPOPO aapa kuapambana kati kati mwa Mji wa Goma na waasi wa M23 wanao ungwa mkono na jeshi la Rwanda

JANUARI 26, 2025
Border
news image

Akizungumuza na wanahabri baada ya mkutano wa kiusalama Generali Ekuka Lipopo Gvana kwa Muda wa Kivu Kaskazini aonya waasi wa M23 kuto subutu kuingia Mjini Goma kwakuepuka maafa mabaya na makubwa Mjini Goma .Ekuka amesema jeshi la Congo FARDC ,Polisi ya DRC na wananchi wata jumhika kwa ajili ya kakabiliana na uasi wa M23 ambao ansema ni jeshi la Rwanda linalo taka kuivamiaa DRC.

Lakini hata hivyo Naibu gavana na gavana kwa Muda amesema Gavana wa Kivu Kaskazini Meje Generali Peter Cirimwami alifariki Dunia kwa majiraha baada ya kupigwa risasi ilio toka eneo la waasi wa M23 wakati alipo kuwa akishinikiza vingozi na wanajeshi kwenye uwanja wa mapigano magharibi mwa Mji wa Goma eneo la kasengezi ikiwa katibu na Mji wa Sake.

Huku hali ya wasiwasi ikiwa kubwa na wafanya kazi wa mashirika ya kimataifa wakianza kuondoka Mjini Goma kwa hofu ya kutokaea mapigano mabaya na silaha zikiwa nyingi Mjini Goma katika Mikono ya raia Pamoja na uwepo wa wanajeshi wengi.

Kwa nyakati za mchana gari ya umoja wa mataifa imeshambuliwa na waasi wa M23 na kusababisha vifo vya askari wa 2 na wengine nne kujeruhiwa .

Mji wa Goma kwa sasa ukiwa katika Gisa kwa ukosefu wa umeme ambao ilikatika wakati wa mapigano ,ukosefu wa umeme ambao waweza leta hathara kubwa na kusababisha vifo katika hospitali mbali mbali na kusimamisha baadhi ya shughuli.

AM/MTV News DRC