TANZANIA

Galacha wa Filamu Bollywood Atua Nchini Tanzania Kufanya Royal Tour

SEPTEMBA 20, 2023
Border
news image

Msanii maarufu duniani kutoka kwenye kiwanda cha filamu nchini India maarufu kwa jina la Bollywood, Sanjay Dutt, akiwa na filamu zaidi ya 200 na tuzo zaidi ya 23 na ikiwa mwaka jana 2022 ametajwa kuwa mmoja wa wanafilamu 3 wa India wenye mauzo mengi (Highest Grossing Indian Films), baada ya kuwasili nchini sasa kuanza rasmi “Royal Tour” kwa kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini Tanzania.

Wakati baadhi ya waigizaji aliowakuta wa zama hizo katika kiwanda cha Bollywood kama Mithun Chakroboti, Amita Bahchan, Shashi Kapoor na Govinda, wakiwa wameondoka katika kiwanda hicho, Sanjay bado amesimama juu kilele akiwa na akina Shah Rukh Khan kupelerusha kiwanda cha filamu za India na hivi karibuni jarida la Filmfare lilimtaja katika 20 Bora ya “100 Years of Hindi Films.”

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania