DRC

DRC wanafunzi wa shule ya msingi waanza rasmi mimtihani ya serikali.

MEI 06, 2024
Border
news image

Ni katika mazingira ya Wasi wasi na vita ndipo wanafunzi wa shule za kiprimary kote nchini Congo mimtihani ya kiserikali imeanza kote.

Eneo la mashariki mwa taifa la DRC kukiwa sintofahamu kutokana na vita vya M23 na Beni wakaazi wakikimbia vijiji vyao kutokana na mauaji ya wapiganaji wa ADF na shule kadhaa zikiwa zimesha fungwa.

Wanafunzi wengine kutoka eneo la vita wakiwa kambini bila kusoma na wengine wakiwa wamesha jiorozesha katika shule kwenye yenye usalama kama Goma na sehemu nyingine.

Huku wanafanzi wanao patikana eneo linalo dhibitiwa na M23 wakishindwa kuendesha mtihani kwani serikali ilisema eneo hilo halipo chini ya uongozi wao na ni vigumu kupeleka mimtihani eneo hilo ambako hawana uhakika wa Usalama.

Wanafunzi wilayani Rutshuru walio kwenda shuleni walionekana wakirudi nyumbani wakiwa na hathira kutoshiriki Mitihani pamoja na wengine.

AM/MTV DRC ONLINE