DRC MUTAA WA LUBERO

Wapiganaji wa Zamani Walio Tiya Chini Silaha Zao na Wanao Kuwa Kwenye Kotuo cha Usalimishaji cha Kasando Walalamika Kuondoka Kituo Hicho

JANUARI 18, 2024
Border
news image

Wapiganaji hawa ambao wana subiri programe ya kuwa rejesha katika maisha ya kirahiya P-DDRCS wakiwa kwenye kituo cha kasando mutaani lubero, walalamika kuondoka kwenye kituo hicho ikiwa serekali ya Drc ha ijibu kwa madai yao, hawa waendeleya kupitiya kipindi kigumu cha maisha kwenye kituo hicho .

Mutafahamu ya kwamba, imepita karibu miezi tisa Wapiganaji hawa wanaonekana kwenye center hiyo wakisubiri kusalimishwa na programe husika P-DDRCS

Jambo wanalo nungunikiya, ni kuona ya kwamba, siku kaza zimemalizika wakiwa hawa pate viakula Jambo ambalo lime endeleya ku wasukuma kuiba mazao shambani mwa wakaaji tendo wasilo furahishwa nalo Wapiganaji hawa . Evariste Kasereka akiwa kiongozi wa P-DDRCS eneo la Butembo na Lubero atibitisha habari hii akinena ya kwamba ni karibu miezi tatu Wapiganaji hawa wana ishi ndani ya Ukosefu wa viakula Jambo linalo endeleya kuwa kera mioyo .

Kiongozi huyu anena kwamba Jambo hilo la Ukosefu wa chakula kwenye kituo hicho, litaweza shurulijikiya kwa ngazi za taifa kupitiya viongozi wa P-DDRCS ili suluhisho ipatinane haraka iwekekanavio.

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS