DRC

DRC Mahakama ya kijeshi yawahukumu kifo wanajeshi walio kimbia vita wilayani Masisi.

MEI 06, 2024
Border
news image

Wakaazi katika Mji wa Goma Kivu Kaskazini waomba sheria kuhusu huku ya Kifo ienze kutekelezwa katika jeshi la Congo FARDC hasa makamanda wanao sababisha wanajeshi kukimbia mapigano.

Akizungumuza na MTV News DRC mmoja wa Vijana wa Lucha asema muda sasa umefika kwa Rais wa Congo Pamoja na mahakama kutekeleza sheria ya kuwauwa watu wanao shiki uasi na kuwaachia nafasi waasi wa mM23 ,hasa wanajeshi ambao kwa sasa washutumiwa kukimbia mapagano wilayani Masisi ambako M23 inaendelea kuchukuwa vijiji.

Mwishoni mwa wiki Mahakama ya kijeshi Mjini Goma iliwahukumu Kifo maofisa nane wa jeshi la Congo FARDC kwakukimbia Vita sake wilayani masisi.miongoni mwao tatu waliachiliwa kwakukosa sababu ya shutuma dhidi yao ,walio hukumiwa wakiomba kukata Rufaa kabla ya siku tano.

Wananchi wa Congo wamekuwa wakishutumu wanajeshi kuwapa nafasi waasi wa M23 kuchukuwa eneo wilayani Masisi na Rutshuru na kusababisha wakaazi kukimbia vijiji vyao na kuwa wakimbizi wa ndani katika taifa lao. M23 imekuwa ikiomba mazungumuzo kama njia moja ya suluhisho la mzozo mashariki mwa Congo swala ambalo serikali ya Kinshasa imekuwa ikisema haiwezekani hata Kidogo.

Ufarasa iliomba Congo na Rwanda kukaa kwa meza moja kutatua shida la usalama mashariki mwa Congo .ila serikali ikisema haiwezi zungumuza na M23 japo inaendelea kuchukuwa vijiji .

AM/MTV DRC ONLINE .