DRC

DRC KATIBU MKUU WA SADEC AOMBA WANANCHI NA VYOMBO VYA USALAMA VYA CONGO DRC KUUNGA MKONO VIKOSI VYAKE

JANUARI 22, 2024
Border
news image

Eliace Magosi Katibu mkuu wa jumhia ya mataifa ya kiuchumi ya kusini mwa Africa SAEDEC asema kwa sasa Jumhia hiyo imekuja mashariki mwa Congo Hasasa Kivu Kaskazini kwa sasa kwa ajili ya kuwapa usalama na Amani wananchi wa Eneo hilo la Mzozo wa Muda mrefu.

Eliace amekutana kwanza na gavana wa Kijeshi wa Kivu Kaskazini Piter Chirimwami na baadae kamanda wa jeshi la ARDHINI na mkuu wa operesheni za kijeshi Kivu Kaskazini na Kivu Kusini Luteni Generali FALL SIKABWE .FALL ameomba wananchi walio kimbia mapigano kuwa watulivu kwani sasa siku za hesabiwa ili warudi kwenye vijiji vyao kwani jeshi la Congo FARDC litashirikiana na SADEC kuhakikisha usalama wa wakaazi unapatikana.

Jeshi la SADEC liliwasili tangu Decemba elfu mbili ishirini na tatu pale askari wa EAC yaani Africa mashariki walianza kurudi nyumbani kwao kutokana na hitilafu na wananchi ambao walishutumu wanajeshi hao kushirikiana na M23 japo walitegemewa sana na wakaazi wengi.

Wachambuzi wa maswala ya kiusalama wasema Congo lazima kujitegemea kuliko kutegemea wanajeshi kutoka mataifa ya kigeni kwani Ni muda mrefu MONUSCO yaani jeshi la Umoja wa Matifa wako DRC kwa Zaidi ya miaka ishirini bila mafanikio.

SAEDEC kwa upande wake wamesema wana Imani kwamba misheni yao haitashindwa na hawashinwi chochote .

AM/MTVONILINE