DRC

DR Viongozi wa Africa waombwa kushughulikia amani na usalama mashariki mwa Congo.

APRILI 23, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV akiwa katika kambi ya wakimbizi ya Bulengo Mjini Goma ,Ema Nyerere asema mateso yamezidi lazima kuyakomesha kwa haraka kwani Watoto na wanawake ndio waathirika wa kubwa katika vita visivyo eleweka ,vita vinavyo sababisha maelfu ya watu kuhama makaazi yao.

Kwa upande wa wanawake wa DRC ,ni muhimu wanao fanya vita kuwaelezea raia wa Congo sababu kubwa ya vita dhidi ya Congo kwani mazungumuzo na makubaliano yamefanyika mengi bila suluhisho,Rwanda ikisema DRC kuna waasi wake ambao ni tishio kwa taifa la Rwanda yaani FDLR swala linalo teremusha mate miongoni mwa wakaazi . Wakimbizi katika kambi mbali mbali kwa upande wao wakisema kwa sasa wanahitaji kurudi nyumbani kwao kwani hawana Chakula na huduma nyingine Muhimu hasa Dawa.

Ema Nyerere Ametembelea Mji wa Goma mashariki mwa Congo kutazama hali halisi kwa wanawake na Watoto wanao patikana katika kambi mbali na kuelewa nini kifanyike kwa haraka ili wanawake na Watoto mayatima na wajane warudi kwenye vijiji vyao.wengi wakiishi kama Wanyama katika hema ambako wanyeshewa na mvua kali na matatizo mengine.

AM.MTV DRC ONLINE