TANZANIA

Dkt Mambosasa Afurahishwa na Mwitikio wa Wananchi Polisi Jamii DPA Cup Awaita Kutumia Viwanja vya Kisasa

SEPTEMBA 20, 2023
Border
news image

Mkuu wa Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam nchini Tanzania (DPA) Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amefurahishwa na mwitikio mkubwa wa timu shiriki na wananchi wanaendelea jitokeza kufuatilia mashindano ya Polisi Jamii DPA Cup yanayoendelea katika viwanja vya chuo cha maafisa wa Polisi Vilivyopo kurasini jijini Dar es salaam.

Dkt Mambosasa ametoa kauli hiyo wakati wa mchezo kati ya TM Rocket na Temeke youth uliomalizika kwa timu ya TM Rocket kushinda vikapu sitini na tano (65) kwa Hamsini na tanu (55) dhidi ya Temeke youth katika mchezo uliyochezwa katika viwanja vya chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) huku akitumia fulsa hiyo kuwakaribisha wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kufika na kutumia viwanja hivyo vipya na vya kisasa vilivyopo chuoni hapo.

Kwa upande wake mchezaji wa timu ya TM Rocket Emmanuel Samiri amesema ushindi wao umechagizwa na mazoezi na mbinu walizofundishwa na mwalimu wao kitendo kilichopelekea kuwachalaza wapinzani wao vikapu (67) kwa Hamsini na tano.

Nae mchezaji wa Temeke youth Paschal Benedicto amesema mchezo wao ulikuwa mgumu kutokana na wapizani wao ambao walikuwa bora Zaidi katika mchezo huku akiwaahidi mashabiki wake kuwa watafanya vizuri Zaidi katika michezo mingine inayofuata.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania