TANZANIA

Dkt. Emmanuel John Nchimbi Ateuliwa Kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa

JANUARI 15, 2024
Border
news image

Chama Cha Mapinduzi kupitia kikao cha Wajumbe wake wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa sauti moja wameridhia na kumpitisha Ndugu. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM - Taifa).

Kikao hicho kimeketi leo tarehe 15 Januari, 2024 Kisiwani Zanzibar kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

CCM inamtakia Dkt. Nchimbi utekelezaji mwema wa majukumu yake mapya.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania